Blog

SOMO: MWAKA MPYA KIWANGO KIPYA


Askofu: Ezekiel Joseph
SOMO: MWAKA MPYA KIWANGO KIPYA

Mstari wa msingi
Isaya 54:1-3, & Kumb 2:1-3

?Katika hazina ya Mungu kuna vitu vingi Sana vya thamani kwa ajili yako, leo tumeuanza mwaka mpya 2020 Lakini mwaka Mpya unaweza ukawa umebadilika ile Namba moja tu badala ya kumi na tisa (19) sasa ni (20), mwaka mpya unaweza usiwe na tofauti kama hautaamua wewe mwenyewe kubadilika, Lazima ufikirie Kutoka katika kiwango hicho na kwenda kiwango kingine.

?Nini maana ya kwenda kiwango kingine?
Tafsiri ya baadhi ya kamusi inasema hiv:-
- Kuzidi wengine
- Isiyo ya kawaida
- Ya kushangaza
Tunapaswa kujua kuwa Mungu hatuwekei mipaka maana yeye mwenyewe anapenda tutoke hapa tulipo na kwenda kiwango kingine kimaisha na kiroho pia, wewe ndio unaweza kujiwekea mipaka ya kwenda kiwango kingine.

(Isaya 43:18 -19) Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.

?Mungu anawazuia wa-Israeli kutokukaa na kuyatafakari mambo ya kale, mambo yale ambayo waliyapitia (Shida/matatizo) Walipokuwa wamechukuliwa kwenda utumwani Misri na Babeli, wanapaswa kusahau kuhusu hayo kwa maana Mungu anaenda kutenda jambo jipya katika maisha yao.

?Fanye kazi kwa bidii na uwe mbunifu kwa kuongeza miradi ili uweze kwenda kiwango kingine cha kimaisha pia weka mikakati ni namna gani unataka kukua kiroho, Baraka zozote za kimwili haziji kimwili tu bali Mungu anataka tunapokwenda kiwango kingine kimaisha iwe kiroho pia, sio mapenzi ya Mungu tubaki katika kiwango kile kile.

?Lakini mahali popote ambapo Mungu anataka kufanya jambo jipya anahitaji mtu ambaye atamtumia ili kuweza kufanikisha hilo, japo haiwi rahisi maana adui hataki wewe utoke hapo na kwenda katika kiwango kingine, anataka uendelee Kubaki hapo hapo siku zote, Wapo baadhi ya wa-Israeli ambao walitaka kusalimu amri kwa Majeshi ya Farao Lakini Musa akawatia moyo Waisraeli;

(Katoka 14:13) Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.

?Hayo ni maneno ya kiongozi mwenye kuwatia nguvu watu wanapopitia katika mazingira magumu, kuna wakati tunajitahidi kutoka tulipokwama na kwenda kiwango kingine lakini tunashindwa na kujikuta tuko pale pale kwasababu kuna adui ambaye hataki utoke hapo, Kama ambavyo ilitokea kwa wa-Israeli ambao majeshi ya Farao yalitaka wasiende kiwango kingine bali waendelee kuwa watumwa wao.

?Haupaswi kabisa kujisalimisha kwa shetani kwasababu ya mazingira fulani unayaona hayawezekani, Mungu anayo njia ktk mazingira hayo.

Mambo ya kuzingatia ili kwenda kiwango kingine;

i) Lazima uelewe wajibu wako katika Kanisa la
mahali pamoja.

Warumi 12:2
?Lakini kuelewa wajibu wako lazima uifanye upya nia yako, maana nia zetu zilikuwa zimeathiriwa na mfumo wa dhambi ambao tuliishi kabla ya kuokoka, lazima uifanye upya Nia yako.
?Kila mwamini ana jukumu la kufanya ktk Kanisa la mahali Pamoja, lakini kwanza Lazima uifanye upya nia yako, ndipo unaweza kuwa mshirika mzuri wa Kanisa la mahali pamoja.

- Tunajifunza kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yetu kupitia mafundisho;
?Unaweza kutaka kufanya maamuzi Mabaya Lakini unapokuja Kanisani na             kusikia neno la Mungu unafanya maamuzi sahihi.

- Kukamilishwa na kukua katika Neno;
?Kupitia Neno Lake Mungu anatutengeneza (kutukamilisha) ili tuweze kufaa kwa     kazi yake, Kukua katika Neno ni kuwa na ufahamu kubwa kuhusu Neno la Mungu.

- Uvumbuzi wa hali katika Maisha;
?Unapokuja Kanisani unaweza kusikia Neno ambalo linaweza kuwa ndio uvumbuzi     wa tatizo ambalo unalo.

- Kukuza huduma na karama yako;
?Katika Kanisa la mahali pamoja tafuta kitu cha kufanya usiwe kama mgeni au         mwalikwa, jihusishe na shughuli mbalimbali hapo, hakikisha kila sehemu katika        maisha yako panakuwa na Ukuaji.

- Ushirika na watakatifu;
?Acha kujitenga na Kanisa maana hapo ndipo unapopatia nguvu Mpya,       unapojitenga na Kanisa unaanza kupoa wakati ulikuwa moto.

- Kutoa zaka na sadaka;
?Kila unapoenda Kanisani jiulize naenda kumwabudu Mungu kwa matoleo gani?      Kutoa sadaka kunaonesha uaminifu wako kwa Mungu lakini pia maana yake     unaunga mkono maono.

?Katika mstari wa msingi Isaya anasema kaza vigingi vya hema yako, imarisha maisha yako acha kuzunguka zunguka mahali pamoja kwa muda mrefu, anza kuchukua hatua ili utoke hapo ulipokwama na kwenda katika kiwango kingine anza mwaka kwa kuamua, maana halifanyiki hali hadi wewe mwenyewe umeamua.
Karibu Beroya tujifunze pamoja No 0755 305794, 0712 623697 & 0783 106865

 

Leave Your Comment